Klabu ya Yanga imetangaza rasmi kumteua Pedro Gonçalves, raia wa Ureno, kuwa Kocha Mkuu mpya wa timu hiyo, akichukua nafasi ya Roman Folz aliyemaliza muda wake klabuni hapo.
Pedro Gonçalves, mwenye umri wa miaka 49, ni kocha mwenye uzoefu mkubwa katika soka la kimataifa. Kabla ya kujiunga na Yanga, Gonçalves aliwahi kuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Angola, ambapo aliongoza taifa hilo kushiriki michuano kadhaa ya kimataifa.
Mbali na hilo, Gonçalves amewahi pia kufanya kazi kama kocha wa kikosi cha vijana cha klabu maarufu ya Sporting Lisbon nchini Ureno — moja ya timu zinazotambulika kwa kukuza vipaji vya wachezaji vijana barani Ulaya.
Uongozi wa Yanga SC umesema unamkaribisha Gonçalves kwa mikono miwili na unaamini ataendeleza mafanikio ya timu hiyo ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Related
