Askofu wa Kanisa la Furahini katika Bwana la jijini Dar es Salaam Dkt.Ezekiel Mwankenja amesema kuwa Watanzania kujitokeza katika kupiga kura Oktoba 29 ili kutimiza haki yao ya kikatiba.
Hayo amesema Dkt.Mwankenja wakati wa Uzinduzi wa Bendi ya Winners ya Kanisa hilo yenye Albam yenye nyimbo 140 ambapo kazi kubwa ni kwa ajili kutoa huduma ya kuinjilisha.
Amesema kuwa watanzania katika kipindi cha uchaguzi ni wajibu wa kulinda amani yao katika kupata viongozi wataoleta marndeleo kwa miaka mitano.
Mwankenja amesema kuwa viongozi wa dini ni wajibu wa kuhimiza waumini kwenda kupiga kura kwa viongozi wao.
Aidha amesema Kanisa hilo kazi yeke kutoa huduma ambapo haiwezi kujitenga na masuala ya kijamii kwa waumini hususani suala la kuchagua viongozi katika uchaguzi wa Oktoba 29 mwaka huu.
“Tunatoa huduma ya kiroho hivyo waumini wetu wanatakiwa kuhimizwa masuala yao ya kushiriki katika kutimiza takwa la kikatiba ikiwemo kushiriki kupiga kura”amesema Mwankenja.
Askofu wa Kanisa la Furahuni Katika Bwana Dkt.Ezekiel Mwankenja akizungumza katika uzinduzi wa Bendi ya Winners ya Kanisa hilo jijini Dar es Salaam.
Askofu Dkt.Mwankenja akiwa na wazee wa Kanisa hilo katika uzinduzi ya bendi ya winners jijini Dar es Salaam .

Baadhi ya matukio katika uzinduzi jijini Dar es Salaam .


