Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi kupitia CCM Azza Hillal Hamad akinadi sera kwa wananchi wa Itwangi.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mgombea Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo jipya la Itwangi, Mhe. Azza Hillal Hamad, amehitimisha kampeni zake leo Oktoba 27, 2025, kwa mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Tinde, akiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura Oktoba 29.
Mkutano huo wa kufunga kampeni umehudhuriwa na maelfu ya wananchi na wanachama wa CCM, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa, aliyeongoza na kuhamasisha wananchi kuichagua CCM katika nafasi zote.
Akizungumza katika mkutano huo, Mhe. Azza ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Shinyanga na hasa katika maeneo yanayounda Jimbo Jipya la Itwangi.
Amesema dhamira yake kama mbunge ni kuendelea kushirikiana na Serikali ya CCM kuhakikisha wananchi wa Itwangi wanaimarishiwa huduma bora za kijamii ikiwemo maji, elimu, afya, barabara na uwezeshaji kiuchumi.
“Nawaomba Oktoba 29 mjitokeze kwa wingi kupiga kura, tuichague CCM kuanzia kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, mimi Azza Hillal Hamad kama Mbunge wenu wa Itwangi, pamoja na madiwani wote wa CCM. Tukifanya hivyo, tutaendelea kupata maendeleo ya kweli,” amesema Azza.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa amewapongeza wananchi wa Itwangi kwa mwitikio mkubwa kwenye kampeni za CCM na kusisitiza kuwa chama hicho kina sera madhubuti zinazotekelezeka na zinazolenga kuinua maisha ya Watanzania.
“CCM ndiyo chama pekee kinachotekeleza ahadi zake. Tumeshuhudia maendeleo makubwa chini ya uongozi wa Dkt. Samia, hivyo tusipoteze mwelekeo, tusimame na CCM,” amesema Mlolwa.
Kufungwa kwa kampeni hizo kunatarajiwa kufuatiwa na siku mbili za maandalizi kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025, ambapo wananchi wa Itwangi wataamua kupitia sanduku la kura, huku Azza Hillal Hamad akipigiwa upatu kuwa mmoja wa wagombea wenye ushawishi mkubwa katika jimbo hilo jipya.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa, akimuombea kura Mgombea Ubunge wa Jimbo jipya la Itwangi, Mhe. Azza Hillal Hamad.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa, akielezea kwa wananchi namna sahihi ya kuwapigia kura wagombea wa CCM katika mkutano wa kufunga kampeni uliofanyika Kata ya Tinde, Oktoba 27, 2025.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa (kulia) akielezea kwa wananchi namna sahihi ya kuwapigia kura wagombea wa CCM katika mkutano wa kufunga kampeni uliofanyika Kata ya Tinde, Oktoba 27, 2025.
Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi kupitia CCM Azza Hillal Hamad akinadi sera kwa wananchi wa Itwangi.
Mgombea Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo jipya la Itwangi, Mhe. Azza Hillal Hamad, akizungumza na maelfu ya wananchi katika mkutano wa kufunga kampeni uliofanyika Kata ya Tinde, Oktoba 27, 2025, ambapo aliwaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kupiga kura Oktoba 29.
Mgombea Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo jipya la Itwangi, Mhe. Azza Hillal Hamad, akizungumza na maelfu ya wananchi katika mkutano wa kufunga kampeni uliofanyika Kata ya Tinde, Oktoba 27, 2025.
Mgombea Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo jipya la Itwangi, Mhe. Azza Hillal Hamad, akiomba kura wakati akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa kufunga kampeni uliofanyika Kata ya Tinde, Oktoba 27, 2025







Mgombea Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo jipya la Itwangi, Mhe. Azza Hillal Hamad, akiomba kura wakati akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa kufunga kampeni uliofanyika Kata ya Tinde, Oktoba 27, 2025.









