…………
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kawe kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Bi Glory Tausi amefunga rasmi kampeni zake za nyumba kwa nyumba kwa kuzitembelea kata za Makongo na Mabwepande.
Glory ameahidi kushirikiana na mamlaka husika kuhakikisha Barabara kubwa ya Mabwepande inawekwa Lami, na ameahidi marekebisho kwa barabara za ndani kwenye kata ya Makongo na Mabwepande pia.
Glory ameahidi pia kuhakikisha wakina Mama na Vijana wanapata mikopo Halmashauri ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Glory ameahidi kuhakikisha wale wote wanaodai Nyaraka za umiliki ardhi yaani Hati wanazipata.


