Mgombea Udiwani wa Kata ya Mkuranga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hamza Mahanaka, amewataka wananchi wa kata hiyo kuwachagua wagombea wote wa CCM ili kuendeleza kasi ya maendeleo katika maeneo yao.
Aidha, Mahanaka amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya Jumatano, Oktoba 29, kutumia haki yao ya kikatiba ya kupiga kura, huku akiwatoa hofu kuwa vyombo vya dola vipo kwa ajili ya kulinda amani na usalama wa wananchi wote.
Amesema kuwa wananchi wanapaswa kujitokeza bila woga, kwani uchaguzi ni fursa muhimu ya kuamua mustakabali wa maendeleo ya eneo lao kwa kumchagua kiongozi sahihi kupitia CCM, chama ambacho kimeendelea kusimamia miradi ya maendeleo na ustawi wa wananchi.