SHIRIKA la Kicheko Africa Foundation limetoa mafunzo ya Afya ya Akili (Mental Health) kwa wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya Elimu ya Juu ili kuwajengea msingi Bora wakujitambua na kuepukana na magonjwa yanayosababishwa na matarajio na tofauti wanazokutana nazo Chuoni.
Akifungua Mafunzo hayo yaliyofanyika katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam, Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC), Dkt.Indiael Daniel Kaaya amesema tatizo kubwa wanafunzi wengi wanatoka kwenye mazingira tofauti na mazingira ambayo wanakuja,kinachoongezeka hasa kuja kwenye mazingira mapya nakukutana na watu wapya wanaowazunguka .
Amesema kwamba kama huwezi kuhimili pressure huwezi kuendana na mazingira ya Ile pressure inayatolewa na watu wa rika lako hii ni kutokana na ugumu wa kiuchumi na kushindwa kupanga bajeti zao za mahitaji ya kila siku
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miradi kutoka Kicheko Africa Foundation ,Jovin Mwehozi amesema Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali wamepata nafasi yakushiriki semina hii ya siku mbili ambayo imeandaliwa na Shirika, ili kujifunza mambo yanayosababisha changamoto ya AFYA ya Akili na kuwatengeneza vijana watakaokwenda kuelimisha wanavyuo wenzao.
Sanjari na hayo,amesema mafunzo hayo yamewaelekeza mambo mengi pamoja na kutambua sehemu ambazo anaweza kupata huduma na kumuona nani na wakati Gani,na tumewatwika jukumu kubwa walezi kuwasimamia vijana tuliowapa mafunzo ili wakasaidie vijana wengine.
Tunaipongeza serikali imefanya kitu kikubwa Kila chuo kina mshauri wa wanafunzi ambaye ni mtaalam na mbobezi na ofisi maalum kwa ajili ya ushauri kwa Wanafunzi kwahiyo vyuo na Kicheko Africa Foundation tutashirikiana na hizo ofisi ili kufikia malengo ili mwanafunzi akifika chuoni awe na uhakika kwamba akimaliza tuwe na kijana ambaye amekamilika kama Dira yaTaifa inavyoelekeza kuwa na kijana mwenye elimu bora anaye jua wajibu na majukumu yake.
Ameeleza kuwa Shirika la Kicheko ni shirika la kijamii lenye malengo yake makubwa yakusaidia watu walioko katika mazingira magumu hasa watoto,vijana na akina mama ambapo lengo hasa ni kuhakikisha ustawi wa jamii katika nyanja zote , tunazingatia sana AFYA na malezi ya watoto,vijana na akina Mama.
Aidha, Mwehozi amesema tumeamua kuwa saidia Wanafunzi wa Vyuo Vikuu ili tuwe na Taifa Bora na lenye AFYA ya Akili.
Mshauri wa wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),Paulina Mabuga amelishukuru shirika la Kicheko Afica Foundation kwa kuwashirikisha kwenye semina kwani Ina manufaa sana kwa vijana kwa kwani inawafundisha vijana wawe mabalozi na wenye tabia njema na ninaamini kupitia mafunzo haya vijana wataweza kuwasaidia vijana wenzao ambao wameingia kwenye matatizo mbalimbali kutokana na changamoto mbalimbali za kimaisha ,elimu na kifamilia zinazopelekea wakawa na msongo wa mawazo.
“Vijana watasaidia vijana wenzao na jamii kuwarudisha katika hali ya kawaida,kwa hiyo Kicheko wamekuwa dira kwa vijana ,wamepata elimu za mada mbalimbali hasa afya ya akili iliyotolewa na daktari aliyebobea katika masuala hayo ili vijana waweze kukabiliana na changamoto ya afya ya akili”,amesema Mabuga
Aliongeza kuwa elimu hiyo itawasaidia kuwaelimisha vijana wenzao wanaokabiliwa na dalili na changamoto ya afya ya akili na ni faraja na msaada mkubwa kwa walezi wa wanafunzi katika vyuo vikuu vya elimu ya juu tumeona kwamba Kuna mkono unasaidia kuwarudisha vijana katika maadili mema na kulijenga Taifa letu wakiwa na akili timamu.
Tunawaomba Kicheko mafunzo haya yawe endelevu ili elimu isambae kwa vijana wengi zaidi na manufaa ya jamii na kwa Taifa kwa ujumla lakini pia elimu hii iwafikirie watu wenye mahiraji maalum maana nao pia wanakumbana na changamoto hii ya Afywbya Akili.
Mwanafunzi wa Stashahada ya Socialojia kutoka Chuo cha Kampala University,Ibrahim Mhagama amesema kupitia mafunzo haya nitakuwa balozi mzuri wa kwenda kuelimisha jamii na vijana wenzangu pamoja na kuwapeleka sehemu sahihi wale wote wanaokabiliwa na changamoto ya afya ya akili

