::::
Jeshi la Polisi mkoa Tarime Rorya imesema Video inayosambwazwa ikionesha watu wakiandamana si ya kweli na kwamba imesambazwa na watu wenye Nia ovu hivyo ipuuzwe.
Kupitia taarifa iliyotolewa usiku huu (Oktoba 27, 2025) na Kamanda wa Polisi, Tarime imesema hali ni shwari na hakuna tukio kama hilo.
Hata hivyo taarifa hiyo imesema wananchi wanaendelea na shughuli zao kama kawaida na usalama umeimarishwa.
