::::::
Kada wa Chama cha Mapinduzi na Mkurugenzi wa Msama Promotion Ndugu Alex Msama amesema kuwa kwa takwimu zilizopo, Mgombea Urais kupitia CCM Dkt Samia Suluhu Hassan atashinda Uchaguzi wa kesho kwa kishindo kikubwa.
Msama amesema hayo kutokanana na takwimu zilizotolewa jana na Katibu Mwenezi wa Chama hicho Ndugu. Kenani Kihongosi kuwa Watanzania Milioni 25 walifuatilia kwa karibu sana Kampeni za Mgombea Urais kupitia CCM Dkt Samia Suluhu Hassan.
Msama ameongeza kuwa na Watanzania wengine zaidi ya Milioni 5 wamefuatilia Kampeni hizo bila kufika kwenye mikutano, hivyo kufanya jumla ya wafuatiliaji wa Dkt. Samia kufikia Milioni 30.
Msama amemaliza kwa kusema kuwa kwa takwimu kama hizo basi Dkt. Samia atashinda Uchaguzi Mkuu kwa kishindo kikubwa na atavunja rekodi kuwa Rais aliyechaguliwa kwa kura nyingi kuliko yeyote yule.