CCM Yafunga Kampeni Kwa Kishindo Uwanja wa Kirumba, Mwanza – Global Publishers

Mwanza, Oktoba 28, 2025 — Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefanya mkutano mkubwa wa kufunga kampeni zake kitaifa katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, tukio lililohudhuriwa na maelfu ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huo na mikoa jirani.

Mkutano huo uliongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akifuatana na viongozi wakuu wa chama na Serikali, wakiwemo mgombea mwenza wa nafasi ya urais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, pamoja na viongozi waandamizi wa chama kutoka ngazi zote.