HATUJASITISHA HUDUMA YA MABASI OKTOBA 29, HAKUNA ALIYEOMBA KIBALI KUSITISHA SAFARI


 ::::::::

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imesema haijatoa kibali cha kusitisha usafiri kwa kampuni yoyote ya mabasi hapa nchini, na kuwatoa hofu wananchi wanaotarajia kusafiri kuendelea na ratiba zao kama kawaida.

Akizungumza kwa njia ya simu na *Torch Media*, Kaimu Mkurugenzi wa LATRA, Johansen Kahatano, alisema ni kweli kumekuwa na taarifa zinazodai huduma za mabasi zimesitishwa, lakini amewasiliana na wahusika na kuthibitisha kuwa huduma hizo zinaendelea kama kawaida.

Aidha, Kahatano alibainisha kuwa mamlaka hiyo haijatoa kibali chochote cha kuzuia safari hizo kwa watoa huduma wa usafiri wa mabasi.

Aliongeza kuwa iwapo kuna mtu au kampuni imeamua kusitisha safari zake kupisha uchaguzi, hiyo ni uamuzi wa mhusika binafsi na si wa mamlaka. 

Kahatano alisisitiza kuwa Jeshi la Polisi tayari limetoa taarifa ya kuwepo kwa hali ya usalama, hivyo wananchi waendelee na ratiba zao kama kawaida.