Dar/mikoani. Shughuli ya upigaji kura katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania kuwachagua madiwani, wabunge na Rais inaendelea huku hali ya utulivu ikitawala.
Laurent Mgumba, mkazi wa Temeke, kata ya Nyambwera, jijini Dar es Salaam akionyesha alama ya wino aliyowekewa katika kidole chake baada ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani leo Jumatano, Oktoba 29,2025. Picha na Aurea Simtowe
Kwa mujibu wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), vituo vilipaswa kufunguliwa saa 1:00 asubuhi na vitafungwa saa 10:00 jioni ya leo Jumatano, Oktoba 29, 2025.
Baadhi ya wananchi wakihakiki majina yao katika Ofisi ya Kata, Mtaa wa Manyimbwi, Wilaya ya Temeke saa 1:18 asubuhi, ambapo wananchi wengine wanaendelea kujitokeza kushiriki hatua ya upigaji kura leo, Oktoba 29, 2025. Picha/Daudi Elibahati
Hata hivyo, baadhi ya maeneo hadi saa 2 asubuhi vituo vilikuwa havijafunguliwa na maeneo megine vilifunguliwa na upigaji kura unaendelea.
Baadhi ya wakazi wa Chatembo, Kata ya Mwandege wilayani Mkuranga, wakihakiki majina yao kabla ya kupiga kura leo asubuhi ya Jumatano Oktoba 29, 2025. Picha na Alawi Masare
Watanzania milioni 37.6 ndiyo waliandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao ndiyo wanaoshiriki shughuli hiyo ya upigaji kura.
Wananchi wakiangalia majina yao katika kituo cha kupigia kura cha sekondari ya Dk Ali Mohamed Shein Jimbo la Kikwajuni Mkoa wa Mjini Magharibi, saa 12:55 asubuhi ya leo Jumatano, Oktoba 29, 2025.
Hali ilivyo kituo cha Haile Selassie, Jimbo la Malindi, Unguja, Zanzibar leo Jumatano Oktoba 29, 2025, saa 12 asubuhi ambapo wapiga kura wemejitokeza kushiriki uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge, wawakilishi na madiwani. Picha na Said Khamis
Endelea kufuatilia Mwananchi.

