October 2025
TARURA Mkuranga Yaendelea na Ujenzi wa Barabara ya Vikindu–Sengetini Kuunganisha Pwani na Dar es Salaam
Na Miraji Msala, Mkuranga – Pwani Mhandisi Aidan Maliva kutoka Kampuni ya Ubaruku Construction Co. Ltd, alisema kazi hiyo inaendelea vizuri kwa kasi na kwa viwango vya juu, huku timu yake ikifanya kazi usiku na mchana kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati uliopangwa. Mradi huu unatekelezwa kwa ubora wa hali ya juu. Tulianza kazi tarehe 20…
Maandalizi ya upigaji kura Kigoma Kusini yakamilika
Uvinza. Wananchi 259,617 wa jimbo la Kigoma Kusini wanatarajia kupiga kura katika uchaguzi mkuu unatarajia kufanyika Oktoba 29, 2025, huku maandalizi yakiwa yamekamilika kwa asilimia mia ikiwa ni pamoja na uwepo wa vifaa vya kupigia kura. Hayo yamesemwa leo Jumapili, Oktoba 26, 2025 na Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kigoma Kusini, Acland Kambili wakati akifungua…
Wagombea urais watakavyopishana kufunga kampeni, kupiga kura
Dar es Salaam. Pazia la kampeni za urais kwa vyama mbalimbali vya siasa linatarajiwa kufungwa katika mikoa minne tofauti, huku wagombea wa nafasi hiyo wakitarajiwa kupiga kura katika mikoa mitano. Mikoa inayotarajiwa kushuhudiwa mikutano ya mwisho ya kufunga kampeni hizo za wagombea hao ni Mwanza, Pwani, Dar es Salaam na Iringa, kwa mujibu wa vyama…
Dk Mwinyi afunga pazia la kampeni, akiahidi neema kwa Wazanzibari
Unguja. Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Hussein Mwinyi, amehitimisha safari yake ya siku 43 kusaka kura za kumrejesha madarakani, huku akiwataka wananchi kumchagua chama hicho, akisema ndicho chenye uwezo wa kusimamia amani na kuleta maendeleo. Mgombea huyo alizindua kampeni za chama hicho Septemba 13, 2025, katika viwanja vya…
Serikali ya Norway yatoa Sh6 bilioni kukuza kilimo cha soya nchini
Dar es Salaam. Ubalozi wa Norway nchini Tanzania na taasisi ya kuendeleza kilimo ya Private Agricultural Sector Support (PASS) Trust wamesaini makubaliano ya kutekeleza mradi wa kuongeza mnyororo wa thamani katika soya ili kuimarisha sekta ya kilimo kupitia ubunifu, fedha jumuishi na teknolojia rafiki kwa mazingira. Makubaliano hayo yaliyofikiwa mwishoni mwa wiki iliyopira ni uthibitisho…
KUJENGA IMANI ZAIDI YA KURA: Jinsi uandishi wa habari kwa kufuata maadili unavyounda mustakabali wa Tanzania tuitakayo
Tanzania ipo katika hatua muhimu sana ya kihistoria, inayokwenda kuunda mustakabali wa Taifa letu. Namna tunavyopitia kipindi hiki, ndivyo tutakavyojenga uimara wa msingi wa maendeleo yetu ya kitaifa katika awamu inayofuata. Chaguzi zinaweza kutugawa, hasa tunapokuwa katika mkondo wa ukuaji unaotia matumaini. Hata hivyo, ni wajibu wa kikatiba unaofanyika kila baada ya miaka mitano na…
UCHAMBUZI WA DANIEL MJEMA: Hii ndio hatari ya Polisi kutotekeleza amri ya mahakama
Oktoba 23,2025, Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Bukoba, kupitia maombi maalumu (Habeas Corpus), ilitoa amri kwa Jeshi la Polisi kuwaachia huru au kuwafikisha kortini, watuhumiwa wa uhalifu wanaowashikilia kinyume cha sheria. Lakini badala ya kutekeleza amri hiyo ya mahakama, tumemsikia na kumuona Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Brasius Chatanda, akijitetea kuwa hawajapokea amri hiyo…
TARURA Kisarawe Yaendelea Kuboresha Miundombinu ya Barabara Kuimarisha Huduma kwa Wananchi
Na Miraji Msala, Kisarawe – Pwani Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani umeendelea kuboresha miundombinu ya barabara kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabara na madaraja, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuboresha huduma…
Profesa Mkenda aahidi kituo cha forodha Tarakea kufanya kazi saa 24
Rombo. Mgombea ubunge wa Jimbo la Rombo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Profesa Adolf Mkenda ameahidi kuwa endapo ataaminiwa tena na wananchi kuendelea kuongoza kwa kipindi kingine cha miaka mitano, atahakikisha kituo cha forodha cha Tarakea kinafanya kazi saa 24 ili kurahisisha biashara za mpakani na kukuza uchumi wa eneo hilo. Akizungumza leo Jumapili, Oktoba…