Dk Mwinyi: Msidanganyike kujitokeza siku ya kura ya mapema
Unguja. Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Hussein Mwinyi amewasihi wananchi wasidanganyike kujitokeza siku ya kura ya mapema kwani walengwa wanafahamika. Kadhalika, amewataka wanachama wa chama hicho, wasibweteke kujiaminisha kuwa tayari wameshashinda, badala yake wajitokeze Oktoba 29, 2025 kukipigia kura chama hicho ili washinde kwa kishindo. Kura ya mapema…