Watatu walioshtakiwa kumuua bodaboda wahukumiwa kifo
Arusha. Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Geita, imewahukumu watu watatu adhabu ya kunyongwa hadi kufa baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la mauaji ya dereva bodaboda. Waliohukumiwa adhabu hiyo ni Faraji Liyugana, Said Ponera na Rashid Fussi ambao walishtakiwa kwa mauaji ya Fanyeni Adam, kosa walilolitenda kinyume na kifungu cha 196 na 197 cha Kanuni…