Msiwatishe wachezaji kwenda Yanga, Simba
MCHEZAJI anapotoka timu nyingine ya hapa nchini na kujiunga na Yanga au Simba kumekuwa na maneno mengi ya kuonyeshwa kwamba anaenda katika hizo klabu mbili kusotea benchi. Lengo hapo ni kutaka kuaminisha kwamba mchezaji anatakiwa kubaki katika timu ya daraja la kati au la chini kiuchumi ili apate nafasi ya kucheza na sio kufuata hela…