Bado Watatu – 46 | Mwanaspoti
NIKAIPOKEA ile simu huku nikiendesha gari nikijua fika kwamba kwa kachero kama mimi kitendo hicho kilikuwa kosa, lakini mapenzi ni kitovu cha uzembe. Nikakikumbuka kitabu cha Ngoswe.“Hello baby…!”“Hello. Habari yako?” Sauti ya Hamisa ikasikika kwenye simu. Ilikuwa kama muziki masikioni mwangu.“Nzuri. Unaendeleaje?”“Sijambo, sijui wewe?”“Mimi nashukuru Mungu. Niambie…?”“Leo niko ‘off’. Nimepumzika nyumbani,” akaniambia.“Upo nyumbani?” nikamuuliza kama…