Wanne wafariki akiwemo Ofisa elimu, ajali mbili tofauti Songwe
Songwe. Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe limethibitisha kutokea kwa ajali mbili mfululizo zilizopoteza maisha ya watu wanne na kujeruhi watano, baada ya magari mawili kugonga tela la Lori lililokuwa limeharibika na kuegeshwa barabarani. Ajali hizo zilitokea Septemba 29, 2025 saa 5 usiku katika eneo la Hanseketwa, Kata ya Ihanda, Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe….