Tumia mbinu hizi kuzuia wivu, migogoro ya watoto
Uhusiano mzuri kati ya ndugu, ni msingi muhimu wa amani na umoja katika familia. Watoto wanaokua katika mazingira yenye upendo na mshikamano huwa na uwezekano mkubwa wa kuwa watu wenye huruma, uvumilivu na heshima wanapokuwa watu wazima. Hata hivyo, wivu na migogoro kati ya ndugu ni mambo ya kawaida yanayotokea katika familia nyingi, hasa pale…