HESLB yatoa Sh426.5 bilioni kwa wanafunzi 135,240 wa elimu ya juu
Arusha. Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa mikopo na ruzuku yenye thamani ya Sh426.5 bilioni kwa wanafunzi 135,240 wa elimu ya juu nchini kwa mwaka wa masomo 2025/2026 ikiwa ni awamu ya kwanza ya upangaji wa mikopo na ufadhili wa Samia Scholarship. Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Oktoba…