Kampeni za udiwani Kirua Vunjo Magharibi zatishiwa kufuatia kifo cha mgombea
Moshi. Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imesitisha shughuli zote za kampeni za uchaguzi wa udiwani katika Kata ya Kirua Vunjo Magharibi, Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro, kufuatia kifo cha mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), John Kessy. Kessy alifariki dunia Oktoba 21, 2025 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa ya Mawenzi iliyopo…