Dakika 810 zamtosha Malale Mbeya City, atemwa na wenzake kikosini
Baada ya kuitumikia Mbeya City kwa takribani miezi nane pekee, Kocha Mkuu, Malale Hamsini na wenzake wa benchi la ufundi wamesitishiwa mkataba leo Jumapili Novemba 30, 2025. Hii ni baada ya matokeo yasiyoridhisha katika mechi tatu mfululizo timu hiyo ikipoteza dhidi ya Mashujaa bao 1-0, Coastal Union (2-0) na Namungo (1-0). Hata hivyo, katika hali…