Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limetangaza nafasi za ajira katika kada tofauti likiwaalika Watanzania wenye sifa stahiki kutuma maombi yao.
Lengo ni kuongeza nguvu kazi na kuboresha utendaji wa sekretarieti ya Bunge.
Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa jana Jumatano, Novemba 5, 2025 na Katibu wa Bunge, nafasi hizo zimeundwa kwa mujibu wa Ibara ya 62(1) na 88(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambazo zinalipa Bunge mamlaka ya kuwa na sekretarieti yake yenye jukumu la kuliwezesha kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Nafasi zilizotangazwa ni pamoja na Mkutubi Daraja la II (nafasi 2), Fundi Sanifu Mifumo ya Maji Daraja la II (2), Mtakwimu Daraja la II (2), Ofisa Ugavi Daraja la II (1), Ofisa Sheria Daraja la II (3), na Ofisa Habari Daraja la II (3).
Nyingine ni Ofisa Tehama (System Administrator) (1), Ofisa Utafiti Daraja la II (3), Mpokezi Daraja la II (4), Ofisa Tehama ( Network Administrator) (1) na Mwandishi Taarifa Rasmi za Bunge (Isimu ya Lugha) (1),
Nafasi zingine ni Mwandishi Taarifa Rasmi za Bunge (Uhazili) (2), Mhasibu Daraja la II (2), na Ofisa Usimamizi wa Fedha Daraja la II (1).
Related
