RAIS DKT. MWINYI AMUAPISHA MWANASHERIA MKUU WA ZANZIBAR

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amemuapisha Dkt. Mwinyi Talib Haji kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.

Hafla ya uapisho imefanyika leo Novemba 6, 2025, Ikulu, Zanzibar.

Dkt. Mwinyi Talib Haji ameteuliwa tena kushika nafasi hiyo baada ya kuitumikia katika kipindi kilichopita.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla, Mhandisi, Zena Ahmed Said, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama Cha Mapinduzi na Dini.