Dodoma. Wakati Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza uteuzi wa wabunge 115 wa Viti Maalumu, Bunge hilo kwa mara nyingine halitakuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni.
Bunge la 12 lililovunjwa Agosti 2, 2025, licha lkuwa na jumla ya wabunge 26 wa upinzani, halikuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani badala yake lilikuwa na kundi la wabunge waliowachache.
Katika Bunge hilo, Viti Maalumu walikuwa 19 kutoka Chadema na wa majimbo wakitoka vyama vya ACT-Wazalendo, CUF na Chadema pia.
Hali hiyo inaendelea kwenye Bunge la 13 ambalo lina idadi ndogo zaidi ya wabunge wa upinzani, wakiwa 12 pekee, wa majimbo 10 na Viti Maalumu wawili.
Kambi Rasmi ya Upinzani kwa mujibu wa kanuni huundwa ikiwa idadi wabunge wa upinzani wanaofikia asilimia 12.5 ya wabunge wote.
Sehemu ya tano ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la 2023, katika kifungu 21, inasema: “Wabunge wa vyama vyenye wabunge walio wachache bungeni wanaweza kuunda kambi rasmi ya walio wachache bungeni iwapo idadi yao itakuwa chini ya asilimia 12 na nusu ya wabunge wote,” inasomeka kanuni hiyo.
Katika orodha iliyotolewa na INEC leo Ijumaa Novemba 7, 2025, jumla ya wabunge wa Viti Maalumu 115 wameteuliwa wakiwemo Devotha Minja na Sigrada Mligo ambao wameteuliwa kutoka Chaumma.
Wengine ambao majina yao yamechomoza ni waliokuwa wabunge 19 waliofukuzwa na Chadema na kuhamia CCM kwa nyakati tofauti, akiwemo Salome Makamba na Cesilia Pareso.
Katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025, Devotha alikuwa mgombea mwenza wa urais wa Chaumma. Mgombea wake wa urais alikuwa Salum Mwalimu na chama hicho kilishika nafasi ya pili kwenye matokeo.
Devotha si mara ya kwanza anakuwa mbunge wa viti maalumu kwani mwaka 2015-2020 alikuwa na nafasi kama hiyo kupitia Chadema.
Mligo yeye kwenye uchaguzi mkuu huu alikuwa mgombea ubunge wa Njombe Mjini. Kabla ya kuhamia Chaumma naye alikuwa Chadema, akiwa katibu mwenezi wa Baraza la Wanawake (Bawacha).
Orodha ya walioteuliwa na INEC
Orodha kamili ya wabunge 115 wa Viti Maalumu walioteuliwa na INEC, wamo wabunge 113 kutoka CCM.
Kutangazwa kwa wabunge hao ni kufuatia masharti ya Ibara ya 66(1)(b) na 78(1) za Katiba ya mwaka 1977, pamoja na kifungu cha 112 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani ya mwaka 2024.
“Uteuzi wa mbunge mmoja aliyesalia utafanyika baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa ubunge majimbo ya majimbo la Fuoni (Zanzibar) Siha (Tanzania Bara),” taarifa ya INEC imeeleza.
Walioteuliwa ni Agness Hokororo, Agness Marwa, Aisha Mduyah, Amina Ali Mzee, Amina Said, Amina Iddi Mabrouk, Asha Feruzi, Asha Rashid, Asha Baraka na Asha Motto.
Wengine ni Asya Khamis, Asya Sharifu Omar, Athumini Omary Mapalilo, Aysharose Ndogholi Mattemba, Aziza Sleyumu Ally,
Mbali na hao, wamo Bonnah Kamoli ambaye aligombea ubunge Segerea, Catherine Canute Joachim, Chiku Athman Issa, Christina Christopher Mnzava na Cecilia Paresso ambaye pia aliwahi kuwa mbunge wa viti maalumu kupitia Chadema.
Pia, wamo akina Christina Mndeme, Devotha Daniel Mburarugaba, Esther Midimu, Esther Malleko, Fatma Ally Rembo, Ghati Chomete, Grace Elias Mkoma, Halima Bulembo, Halima Iddi Nassor na Happiness Ngwado.
Wengine ni Hawa Mchafu, Husna Sekiboko, Jacqueline Mzindakaya, Jacqueline Andrew, Jacqueline Ngonyani (Msongozi), Jamila Mahmoud Juma, Janeth Mahawanga na Janeth Pinda.
Vilevile INEC imemteua Jasmine Ng’umbi, Jesca Magufuli, Jesca Mbogo, Josephine Kapoma, Josephine Tabitha Chagula, Juliana Shonza, Kabula Shitobela na Khadija Hassan Aboud.
Pia, wameteuliwa Khadija Shaaban ‘Keisha’, Kijakazi Yunus Latifa Khamis Juwakali, Lucy Mwakyembe, Lucy Kombani, Lulu Mwacha, Magreth Ezekiel, Mariam Ibrahim na Mariam Mungula.
Sambamba na hao, pia wamo Mariam Nyoka, Mariam Ussi Yahya, Marirta Gido Kivunge, Martha Festo Mariki, Martha Gwau, Mary Masanja, Maryam Azani Mwinyi na Mary Chatanda ambaye ni mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT-Taifa).
Aidha yupo Maryprisca Mahundi, Mgeni Hassan Juma, Mvita Mustafa Ali, Mwanaenzi Hassan Suluhu, Mwanahamisi Athumani Munkunda, Mwanaisha Ng’anzi Ulenge, Mwantatu Mbarak Khamis, Mwantumu Mzamilu Zodo, Nadra Gulam Rashid na Najma Murtaza Giga.
Pamoja na hao, wamo Nancy Nyalusi, Naomy Mwaipopo, Nasriya Nassir Ali, Neema Mwandabila, Neema Majule, Neema Mgaya, Ng’wasi Kamani, Nyamizi Mhoja, Pindi Chana, Rahma Riadh Kisuo, Rebeca Nsemwa na Regina Malima.
Wengine ni Regina Mikenze, Regina Ndege Qwaray, Rose Tweve, Salome Makamba, Samira Khalfani Amour, Santiel Eric Kirumba, Selina Kingalame, Shadya Haji Omar, Sheila Edward Lukuba, Sikudhani Yassini Chikambo, Stella Ikupa , Suma Fyandomo na Sylivia Sigula, Tamima Haji Abass.
INEC imewateua pia Taska Mbogo, Tauhida Gallos, Timida Fyandomo, Tinnar Chenge, Tunu Kondo, Ummy Ndeiriananga, Yumna Omar, Yustina Rahhi, Zainab Katimba, Zainab Issa, Zainab Kawawa, Zena Katembo, Zeyana Hamid na Zuwena Bushiri.