MWANDISHI WA HABARI SAMSON CHARLES, AWAJIBU WANAOWAKOSOA

::::::

Anaandika, Samson Charles  Mwanahabari,mc na mtangazaji

UZOEFU WA TASNIA YA HABARI MIAKA 15.

Jibu ni rahisi sana.

– Je, wewe ulipoambiwa mwisho wa kuonekana nje ni Jumatano saa 12 kamili jioni ulionekana? 

-. Je, ulipoambiwa mwisho wa kufungua duka saa 4 asubuhi halafu ufunge je uliendelea kufungua? 

– Bodaboda walipoambiwa “hakuna kufika mjini mwisho huko huko mitaani ” ,je walienda mjini?

– Ulipoambiwa “tembea na kitambulisho” je ulitembea bila kutambulisho? 

– Kuna muda uliambiwa “kaa ndani usitoe hata pua nje “, je ulitoa pua yako nje?

Sasa kama wewe uliweza kutekeleza agizo, vipi kuhusu sisi wanahabari?😒

UTANIULIZA SWALI ,.JE MEDIA MLIPEWA MAAGIZO? MLIBANWA (Mimi hilo swali sijibu, nakuachia wewe maana najua una D2)

Je mnajua kwamba tunaripoti kwa mujibu wa mamlaka? Au mlitaka sisi twende front then mida hii mseme “Sam alikua shujaa sana ” halafu? 

Si mlisikia tetesi sijui kuna raia wa kigeni wanapita huko wanamiminia watu njugu? So mlitaka mi bila bullet proof nitoke nje na kitambi changu kweli? Mbona wewe ulilala ndani ? Halafu baada ya miezi 9 tukija kukagua tukakuta umezaa/umezalisha itabidi utuambie ulikua unafanya nini wakati nchi ipo kwenye tense.

Issue ni kwamba kabla hujachagua kulaumu, fikiri twice as much kisha laumu.

Pia nikuulize swali lisilo la kizushi, Hivi wewe hii leo ushawahi kwenda kumsalimia mke wa AZORY GWANDA? Je unajua Mwanahabari AZORY GWANDA ambaye hajulikani alipo familia yake inaendeleaje?

Je watoto wa AZORY GWANDA wakija kukuomba ada na kodi ya nyumba utawalipia?

Pichani ni Marehemu DAUDI MWANGOSI ,.mwanahbari wa zamani wa channel Ten aliyefariki dunia September 2 mwaka 2012, sitaki kusema mengi ila apumzike kwa amani.

UJUMBE: Yanga hii unaifungaje?