Washiriki Kili Marathon 2026 Watakiwa Kujiandikisha kwa Wakati – Global Publishers

Waandaji wa Mbio za Kimataifaiza za Masafa Marefu (Marathoni) za Kilimanjaro Premium Lager 2026 wamewasihi washiriki kujiandikisha kwa wakati kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza dakika za mwisho.

Taarifa iliyotolewa na waandaaji hao inasema usajili ulianza tangu 20 Oktoba 2025 kupitia www.kilimanjaromarathon.com na mtandao wa Mixx by Yas kwa kupiga *150*01# na kufuata maelekezo.

“Hii itakuwa kwa makundi yote ya mbio, zikiwemo za kimataifa za Kilimanjaro Premium Lager kilomita 42 (mbio kamili za masafa marefu), za kilomita 21 za Yas Kili nusu marathoni) na za CRDB za kilomita 5 za burudani,” inasema sehemu ya taarifa ya waandaaji.

Kwa mujibu wa Kanuni Rasmi za Riadha Duniani zinazolinda usalama wa washiriki kwa mwenyeji wa tukio, kanuni kali zinahitajika kuzingatiwa na hii inamaanisha, usajili wa washiriki wa mbio hizo utafungwa rasmi ama Februari 26 2026 au mapema zaidi, ikiwa tiketi zitauzwa na kumalizika kabla ya tarehe iliyotajwa.

Hii, taarifa inaeleza, ni kwa ajili ya kuhakikisha wanariadha wanafurahia muda wao nje ya safari bila kuwa na msongamano mkubwa, na kwamba vifaa vyote kwa upande wa maji na msaada wa matibabu unaohitajika hadi mwisho vinatayarishwa kwa ufanisi.

Kwa siku yenyewe ya Mbio za Kimataifa za Masafa Marefu, waandaaji wanatoa wito kwa washiriki kuzingatia mabadiliko ya tarehe kutoka Jumapili ya mwisho ya Februari au Jumapili ya kwanza ya Machi kama ilivyozoeleka na sasa mbio hizi zitafanyika 22 Machi, 2026 ili waweze kupanga safari zao ipasavyo.

“Kuna wanaohitaji kushika nafasi ya malazi na kufanya maandalizi mengine, hivyo tunatoa wito kwa washiriki wote kuzingatia tarehe mpya ya toleo la mwaka ujao,” inasomeka sehemu ya taarifa ya waandalizi.

Kilimanjaro Premium Lager ndio wadhamini wakuu wa mbio za kimataifa za masafa marefu na imeshika nafasi hiyo tangu kuanzishwa kwa mbio hizo miaka 24 iliyopita.

Wadhamini wengine kwa mwaka ujao ni pamoja na YAS (kilomita 21 za nusu marathoni), Benki ya CRDB kilomita 5 za burudani.

Wadhamini rasmi wanaounga mkono – Kilimanjaro Water na TPC Sugar. Wabia rasmi – GardaWorld Security, Toyota Tanzania, Columbia Sportswear, Simba Cement na ALAF Limited. Wasambazaji rasmi – Salinero Hotel, Kibo Palace Hotel Arusha na Keys Hotel, Moshi.

Mbio za kimataifa za masafa marefu zinaandaliwa na Kilimanjaro Marathon Company Limited kila mwaka.