Mfanyabiashara na mtangazaji wa mitandaoni, Jenifer Bilikwiza Jovin maarufu Niffer, amepewa mashtaka ya uhaini na kusomewa mahakamani, hatua inayohusiana na vurugu zilizotokea kabla na wakati wa uchaguzi mkuu. Niffer alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu pamoja na washitakiwa wengine 21, ambapo serikali ilimsomea mashtaka matatu yanayohusiana na njama za pamoja za kuharibu utaratibu wa uchaguzi.
Msikilize Wakili Peter Kibatala akifafanua kwa kina mashtaka yanayomkabili mfanyabiashara Jennifer Jovial almaarufu Niffer hapa chini
Related
