Rais wa Rwanda, Paul Kagame, ametupilia mbali madai yanayoenea kwamba anamuandaa mmoja wa watoto wake kuchukua nafasi yake ya Urais baada ya kuondoka madarakani.
Akizungumza jijini Kigali, Kagame alisisitiza kuwa watoto wake ni Wanyarwanda kama wananchi wengine na hawana upendeleo wowote wa kisiasa kutokana na kuwa watoto wa Rais.
“Watoto wangu ni Wanyarwanda kama wengine, wanapaswa kuishi maisha yao ya kawaida. Siwezi kumtafutia mtu Urais, hata huyo mnayemtaja huenda hataki kabisa kuwa Rais,” alisema Kagame.
Rais Kagame, ambaye ameiongoza Rwanda kwa miaka kadhaa tangu kumalizika kwa mauaji ya kimbari mwaka 1994, ameendelea kuwa sauti yenye ushawishi mkubwa katika siasa za ndani na za kikanda, akisisitiza kila mara umuhimu wa utawala wa sheria na maendeleo ya wananchi wote.
Related
