Mhe. Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameapishwa kwa mujibu wa Ibara ya 59(5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 inayompa Mamlaka ya kuwa Mbunge na kuhudhuria vikao vya Bunge.
Aidha, Uapisho huo mbele ya Bunge wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, unafuatia Uteuzi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kumteua Mhe. Hamza S. Johari kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali mnamo tarehe 3 Novemba, 2025 na kufuatiwa na uapisho uliofanyika tarehe 5 Novemba, 2025 Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma.
