Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu, ametangaza kuwa kesho tarehe 13 Novemba 2025, Bunge la 13 katika Mkutano wa Kwanza, Kikao cha Tatu, litakuwa na shughuli muhimu ya kuthibitisha uteuzi wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sambamba na uchaguzi na uapisho wa Naibu Spika wa Bunge.
Mhe. Zungu ametoa kauli hiyo leo, tarehe 12 Novemba 2025, wakati akiahirisha kikao cha pili cha Bunge, Jijini Dodoma. Amesisitiza kuwa ni muhimu kwa wabunge wote kuhudhuria kikao hicho bila kukosa, kutokana na uzito wa ajenda zilizopangwa kujadiliwa.
Ikumbukwe kuwa Bunge hili la 13 lilianza Jumanne, tarehe 11 Novemba 2025, likianza na uchaguzi wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kisha kiapo cha uaminifu na ahadi ya uzalendo kwa wabunge wateule, zoezi ambalo limehitimishwa siku ya leo.
Related
