Lamine Yamal ameondolewa kwenye kikosi cha Uhispania – Global Publishers



Nyota wa klabu ya Barcelona, Lamine Yamal, ameondolewa kwenye kikosi cha Uhispania kwa ajili ya mechi za kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Georgia na Uturuki, chini ya kocha Luis de la Fuente.

Yamal, ambaye alitarajiwa kucheza michezo hiyo baada ya kuiongoza Barcelona kushinda 4-2 dhidi ya Celta Vigo Jumapili, sasa atakosa nafasi hiyo kutokana na jeraha la paja.

Kocha wa Barcelona, Hansi Flick, amewahi kuikosoa timu ya taifa ya Uhispania kwa kumchezesha Yamal katika michezo ya kufuzu mwezi Septemba, jambo lililochangia kijana huyo kukosa mechi nne za Barcelona baada ya kupata jeraha kipindi hicho.

Kwa sasa, Barcelona wamesema kuwa mchezaji huyo atapumzika ili kupona vizuri kutokana na jeraha hilo “gumu” wakati wa mapumziko ya kimataifa.