UJUMBE KUTOKA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI UKIONGOZWA NA BALOZI MEJA JENERALI WILBERT AUGUSTINE IBUGE WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO NGORONGORO.

Na Mwandishi Wetu, Karatu

Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi ( NDC) Balozi Meja Jenerali W.A. Ibuge ameongoza wakufunzi na Wanafunzi kutoka mataifa 17, kutembelea eneo la Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwa kuanzia jengo la makumbusho ya Jiopaki ( Urithi Geo- Museum) kwa ziara ya utalii na kimafunzo.

Ujumbe huo umejifunza mambo mbalimbali kuhusu vivutio vya utalii, shughuli za uhifadhi,  kijiolojia na urithi wa utamaduni yanayopatikana katika eneo la Ngorongoro na maeneo yanayozunguka hifadhi hiyo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Balozi Meja Jenerali Ibuge alisema:

“Tumefurahi kutembelea makumbusho haya ya kipekee na kisasa ambayo yanaonesha utofauti na upekee wa Ngorongoro ukilinganisha na maeneo mengine.

Ameupongeza  ongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kazi kubwa ya kulinda  rasilimali za wanyamapori, kuendeleza utalii, na kuchangia kukuza uchumi wa taifa.

Kwa upande wake, Kamishna wa Uhifadhi Abdul-Razaq Badru, wageni hao  amewahakikishia  ushirikiano wa karibu kati ya Mamlaka na Chuo cha Ulinzi cha Taifa na kusisitiza umuhimu wa kuendelea kutembelea hifadhi na kuwa mabalozi wazuri wa Ngorongoro wanaporudi katika mataifa yao.