Kwa mara ya kwanza , ZIKOMO AFRICA AND CARIBBEAN AWARDS 2025 itafanyika Tanzania tarehe 17 Desemba 2025, katika ukumbi wa kifahari wa SUPER DOME, jijini Dar es Salaam.
Tukio hili kubwa linatarajiwa kuvuta hisia za watu kutoka pande zote za Afrika na Caribbean, likiwa na dhamira ya kutambua na kuthamini michango ya watu mashuhuri katika sanaa, muziki, filamu, mitindo, na ubunifu.
Wasanii Maarufu kama Nandy, Marioo na Mbosso waongoza kwa kua na Nominations nyingi kwa Upande wa Tanzania Huku wasanii wapya kama Mex cortez , Dayoo na marleen plastaz wakipata nominations Pia Huku Millen magese akiwa nominated kwenye Tuzo ya Heshima Kama Best Fashion Icon Of the Year.
Red Carpet itaanza kuangaza kuanzia saa 11:30 jioni hadi saa 1:00 usiku (17:30 – 19:00), ambapo mastaa kutoka Afrika na visiwa vya Caribbean wataonyesha mitindo yao ya kuvutia.
Baada ya hapo, main event itaanza saa 1:40 usiku hadi saa 5:00 usiku (19:40 – 23:00), ikihusisha utoaji wa tuzo, burudani, na maonyesho maalum kutoka kwa wasanii wakubwa barani Afrika.
Tanzania inajivunia kuwa mwenyeji wa hafla hii ya kihistoria, ikionyesha ukuaji wa tasnia ya burudani barani Afrika na nafasi yake kama kitovu cha tamaduni, ubunifu na muziki wa kisasa.
Wasanii kutoka sehemu mbalimbali za bara la Afrika wamechaguliwa kushiriki kwenye tuzo hizi kubwa, hasa wale wanaoibeba roho na ubunifu wa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara (Sub-Saharan Africa).
ZIKOMO AWARDS 2025 – Usiku wa heshima, tamaduni, na ubunifu unaounganisha Afrika na Caribbean!

