Daniel Sillo Baran Achaguliwa Naibu Spika wa Bunge la 13 – Global Publishers



Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini, Daniel Sillo Baran

Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini, Daniel Sillo Baran amechaguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo Bungeni, Katibu wa Bunge, Ndg. Baraka Leonard amesema Mhe. Daniel Sillo Baran amepata kura zote zilizopigwa na Waheshimiwa Wabunge 371.

Uchaguzi huo umefanyika wakati wa Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Kwanza wa Bunge la 13 uliofanyika leo Novemba 13, 2025.