Na Mwandishi Wetu
KIONGOZI Mkuu wa Kanisa la Ngurumo ya Upako Jijini Arusha, Nabii Mkuu GeorDavie Moses, ameteuliwa kuwa Mwakilishi na Balozi wa Amani wa Afrika Mashariki kupitia Shirika la Mabalozi wa Amani la Umoja wa Mataifa (UN-PAF) lenye makao yake makuu Jijini New York, Marekani.
Taarifa kutoka Marekani zinaeleza kuwa uteuzi huo ulifanywa rasmi na Mwenyekiti wa Dunia wa UN-PAF, Balozi Kingsley Ossai, ambaye ametuma barua maalumu za utambulisho kwa Serikali ya Tanzania, United Nations Chapter ya Tanzania pamoja na Ubalozi wa Marekani nchini, kwa lengo la kumtambulisha Nabii GeorDavie katika wadhifa wake mpya.
“Tunatambua mchango wa Nabii GeorDavie katika kueneza amani na maendeleo ya kijamii. Tunaamini kama Balozi wa Amani Duniani, ataziwakilisha vema nchi za Afrika Mashariki kupitia Shirika letu,” imeeleza sehemu ya barua hiyo.
Nabii Mkuu GeorDavie, ambaye pia ni mlezi wa JMAT Taifa, amekuwa akihusishwa kwa muda mrefu na shughuli za kijami.
