Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu akitangaza Jina la Waziri Mkuu aliyeteuliwa na Mhe. Rais baada ya kupokea ujumbe maalum kutoka kwa Mpambe wa Rais (ADC) Brigedia Jenerali Nyamburi Mashauri kuhusu uteuzi huo Bungeni leo Novemba 13, 2025.
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua Dkt. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Jina la Mbunge huyo wa Iramba Magharibi limewasilishwa Bungeni kwa ajili ya Waheshimiwa Wabunge kumthibitisha kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

Related
