Waziri Mkuu Mteule Dkt. Mwigulu Nchemba Apokelewa kwa Shangwe Dodoma – Video – Global Publishers



Waziri Mkuu Mteule, Dkt. Mwigulu Nchemba, amepokelewa kwa heshima kubwa na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu katika makazi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, leo Novemba 13, 2025.

Mapokezi hayo yamefuatia uteuzi wake uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, na kuthibitishwa rasmi na Bunge la Tanzania katika kikao kilichofanyika leo asubuhi.

Watumishi wa serikali na viongozi mbalimbali walijitokeza kumpokea Dkt. Nchemba, wakionesha furaha na matumaini mapya kwa uongozi wake.

Dkt. Nchemba, ambaye awali alikuwa Waziri wa Fedha na Mipango, anatarajiwa kuanza majukumu yake mapya mara moja, akiendelea kusimamia utekelezaji wa dira ya maendeleo ya taifa chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.