KAMPUNI inayoongoza katika michezo ya kubashiri nchini, Meridianbet Tanzania, imeendelea kudhihirisha dhamira yake ya kusaidia jamii kwa kutoa msaada wa vyakula na mahitaji muhimu kwa kituo cha MRC Rehabilitation Centre kilichopo Dar es Salaam.
Msaada huo uliojumuisha mchele, unga wa sembe, mafuta ya kupikia, sabuni za kufulia na mahitaji mengine muhimu ya nyumbani, umekabidhiwa rasmi na timu ya Meridianbet kama sehemu ya utekelezaji wa mpango wao wa Corporate Social Responsibility (CSR) wa mwezi Novemba, wenye lengo la kugusa maisha ya watu wanaokabiliana na changamoto mbalimbali za kiafya na kijamii.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, msemaji wa Meridianbet alisema kuwa msaada huo ni sehemu ya jitihada endelevu za Meridianbet katika kuunga mkono taasisi zinazosaidia watu wenye uhitaji maalum.
Meridianbet haikuachi nyuma, kuna michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds bomba zinazokuongezea nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku. Kujiunga ni rahisi! Tembelea meridianbet.co.tz au piga *149*10#.
“Tunatambua umuhimu wa taasisi kama MRC Rehabilitation Centre katika kuwasaidia watu wanaopitia hatua za matibabu ya uraibu. Kama kampuni inayowajibika kijamii, tumeona ni vyema kushiriki katika kuhakikisha wanaoishi kwenye kituo hiki wanapata mahitaji ya msingi kama chakula na usafi,” alisema.
Kwa upande wao, viongozi wa MRC Rehabilitation Centre waliishukuru Meridianbet kwa moyo wa upendo na kujitoa kusaidia jamii, wakieleza kuwa msaada huo umefika kwa wakati ambapo kituo kinahitaji sana rasilimali za kusaidia wahusika wanaopatiwa huduma za ukarabati.
“Tunashukuru sana Meridianbet kwa msaada huu. Umekuja wakati sahihi na utasaidia sana kuhakikisha wale tunaowahudumia wanapata mahitaji ya msingi. Tunathamini sana ushirikiano huu na tunatarajia kuendelea nao,” alisema mmoja wa viongozi wa kituo hicho.
Meridianbet imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia jamii kupitia miradi mbalimbali ya kijamii, ikiwemo kusaidia vituo vya watoto yatima, hospitali, shule, na vikundi vya jamii vinavyolenga ustawi wa wananchi.