Mjumbe Maalumu wa Masuala ya wanawake, Amani na Usalama katika Bara la Afrika, Balozi Liberata Mulamula, amepongeza hotuba nzuri ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan yenye weledi wa kuijenga Tanzania moja kupitia maridhiano.
Balozi Mulamula ameyasema hayo, Leo, jijini Dodoma, aliposhiriki mkutano wa uzinduzi wa Bunge la 13 na kusikiliza hotuba ya Rais Dk.Samia.
“Nimefurahi kuwepo Dodoma kwenye uzinduzi wa Bunge na kusikiliza hotuba ya Mhe. Rais Dk.Samia ilikuwa nzuri na yenye mguso kwa kweli, ikilenga kujenga Tanzania moja yenye umoja na mshikamano na serikali inayochochea maendeleo kwa wananchi,”alisema.
Alisema hotuba hiyo imeonesha namna ambavyo Rais Dk.Samia amekusudia na amejipambanua kujenga serikali rafiki na wananchi na kuwepo maendeleo makubwa ya kiuchumi na Taifa.
Pia, aliwasisitiza wananchi kuendelea kutekeleza wito wa Rais Dk.Samia wa kudumisha amani na utulivua kujenga uchumi na kuwepo maendeleo.
Katika hatua nyingine Balozi Mulamula, alimpongeza Makamu wa Rais Dk.Emmanuel Nchimbi na Makamu wa Rais wa pili wa Zanzibar, Hemmed Abdullah kwa nafasi hizo adhimu.
Aidha, alimpongeza Waziri Mkuu Dk.Mwigulu Nchemba na Spika wa Bunge, Musa Zungu, Naibu Spika, Daniel Sillo, kwa kuaminiwa kutumikia nafasi zao hizo mpyaa, ikiwa ni sehemu ya kuwatumikia wananchi kuchochea maendeleo ya Taifa.
000000


