Faida za tendo la ndoa kwa wanandoa

Nia na madhumuni ya makala haya sio kuchochea ufanywaji wa tendo la ndoa kwa wasio wanandoa, bali kujaribu kuongeza ujuzi na ufahamu na uboreshwaji wa mazingira ya tendo hili kwa wanandoa.

Hii inatokana na ukweli kwamba, kati ya wateja wanaokuja ofisini kwangu (mimi kama mshauri wa kisaikolojia) asilimia zaidi ya 80 hu-susani wanawake wamekuwa wakielezea kutoridhishwa kwao, au uchu wa kutaka kusaidiwa zaidi juu ya maisha na mazingira ya tendo la ndoa.

Jambo hili limeelezwa sana kuwa ndicho chanzo cha misuguano na kupoa au kufa kabisa kwa ladha ya penzi katika ndoa nyingi, nadhani wewe pia waweza kuwa shahidi wa hili. Manufaa haya yatagusa baadhi ya maeneo mbalimbali ya wanandoa husika kama ifuatavyo.

Tendo la ndoa ni moja kati ya mazoezi ya mwili, wataalamu wanasema unapofanya tendo hili kati ya mara tatu au zaidi kwa wiki husaidia kupunguza kiasi kikubwa cha mafuta mwilini.

Tendo la ndoa pia huongeza ta-kribani vizalisha nguvu 150 kwa nu-su saa ambayo ni sawa na kukimbia dakika 15 kiwanjani.

Tendo la ndoa husaidia kuongeza kasi ya mtiririko wa damu kwenye ubongo na sehemu nyingine za vi-ungo vya mwili. Hii huchangia kuongeza kasi ya mapigo ya moyo na kuboresha mfumo wa upumuaji.

Msukumo thabiti wa damu mpya yenye oxygen na homoni zenye chembe chembe hai zinapopenya kwenye mishipa ya damu, husaidia katika uunguzaji wa chakula, pia huondoa kiasi cha uchafu ambao ungesababisha mishipa kushindwa kufanya kazi na kumfanya mwana-damu apate uchovu au maumivu ya mwili.

Tendo la ndoa huweka sawa uwiano wa mafuta yenye kileo yaani lehemu nzuri na mbaya na wakati huo hu-punguza kwa ujumla kiasi cha mafu-ta yenye kileo mwilini.

Wakati wa kufanya mapenzi, homoni iitwayo oxytosin huzalishwa mwilini ambayo husababisha ku-zalishwa kwa homoni iitwayo en-dorphin ambazo hupunguza maumivu kama vile kuvimba se-hemu za viungo maumivu ya shingo na maumivu ya kichwa.

Majimaji yanayozalishwa katika te-zi ya kibofu yakizidi, husababisha kuleta matatizo mwilini. Tendo la ndoa lenye mpangilio huondoa uzalishaji wa maji maji hayo yenye madhara. Mabadiliko ya ghafla ya tendo la ndoa yanaweza kuleta matatizo yahusianayo na tezi ya prostate.

Kupunguza mfadhaiko wa moyo

Kujitosheleza na kupumzisha mwili baada ya tendo la ndoa, ni muhimu kwa kutuliza akili na kurekebisha mzunguko wa damu mwilini.

Watu wenye kushiriki tendo la ndoa vizuri wanatajwa kuushinda mfa-dhaiko na kupata usingizi mnono hasa baada ya kumaliza kufanya tendo hilo.

Katika ufanyaji wa tendo la ndoa, homoni za kiume na za kike hu-zalishwa zaidi na hii huongeza msukumo wa kufanya tendo hilo zaidi na zaidi na mara kwa mara.

Hata hivyo, madaktari wamegundua kwamba ongezeko la homoni za kike na kiume huweza kuwakinga wanadamu na magonjwa ya moyo.

Kuishi muda mrefu huku ukionekana kijana

Wakati wa tendo la ndoa homoni iitwayo DHEA huzalishwa mwili mzima. Hii husaidia msisimko wa mapenzi kuongezeka. Kutokana na elimu hiyo, DHEA ni kemikali yenye nguvu duniani ambayo husaidia kuweka sawa kinga ya mwili, kuongeza ufahamu, huimarisha mifupa, hutengeneza na kuimarisha afya pamoja na kuimairisha mishipa ya moyo.

Kupunguza baridi na mafua

Watafiti wa masuala haya wame-onyesha kuwa wanandoa wanaofan-ya tendo la ndoa mara moja au mbili kwa wiki, huongeza asilimia 30 ya uzalishaji wa chembechembe hai za mwili ziitwazo ‘immunoglonlin’ ambazo huwa na kazi ya kuulinda mwili dhidi ya magonjwa hususani mafua.

Faida hizi huwa thabiti na dhahiri kwa wanandoa zaidi ya wale wasio wanandoa.Hii ni kwa sababu ya mazingira kamili ya tendo la ndoa kwa wanandoa pasipo hofu ya kufumaniwa au kuundiwa kashfa, wala pasipo aina yoyote ya msongo wa mawazo.

Usisahau pia ziko hasara za kufanya tendo la ndoa kwa kupitiliza, ni lazima mke na mume muwe na kiasi.