Steven Waiton Mengele almaarufu kama SteveNyerere2 ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao na Mdau wa maendeleo katika shughuli za kijamii kupitia sanaa za maigizo na uchekeshaji kwa miaka mingi sasa.
Ndugu Steve amekuwa akihakikisha anakuwa daraja la wadau, wasanii na makundi mbalimbali ya wenye uhitaji akiwawezesha kwa namna moja au nyingine katika kupunguza au kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili pale wanapokosa msaada.
Upo ushahidi wa kuwa Steve ni mwenye mchango mkubwa kati ya wengi waliofanikiwa kupata msaada wa hali na mali kupitia jitihada zake hasa jambo likiwa ndani ya uwezo wake kwa kushirikiana na wadau wengine wa ndani na nje ya nchi.
Steve kutokana na nia yake thabiti na kufanikisha mambo makubwa ya kijamii amefanikiwa pakubwa hata kuaminiwa na taasisi, wadau wakubwa, viongozi na jamii kwa kiasi kikubwa kiasi cha kutazamwa kama daraja muhimu kwa Watanzania wengi wenye uhitaji.
Aidha, Steve anafuatiliwa kwa ukaribu kupitia vyombo vya habari na mitandao mbalimbali ya kijamii kutokana na namna yake ya kufanikisha mambo na kusambaza ujumbe pale anapoona kuna uhitaji wa kufanya hivyo.
@mamaongeanamwanao_