TUMEMKAMATA MWANAJESHI WA MAREKANI AKIWA NA MABOMU MANNE


 :::::::

Jeshi la Polisi Tarime Rorya limesema limemkamata Charles Onkuri Ongeta, mwenye umri wa miaka 30 na uraia wa Marekani na Kenya, akidaiwa kuingia Tanzania kupitia mpakani Sirari akiwa na mabomu manne aina ya CS M68.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, mtu huyo anadaiwa kuwa mwanajeshi wa Marekani mwenye cheo cha Sajenti na alikamatwa akitumia gari lenye namba KDP 502 Y aina ya Toyota Landcruiser.