Polisi Waanza Uchunguzi wa Kifo cha MC Pilipili Dodoma – Video – Global Publishers



Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma, kupitia kwa Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Gallus Hyera, amesema linaendelea kufanya uchunguzi kuhusu chanzo cha kifo cha aliyekuwa Mshereheshaji na Mchekeshaji Emmanuel Mathias, MC Pilipili, baada ya kuwepo kwa taarifa zenye utata juu ya mwili wake ikielezwa kuwa umekutwa na majeraha.

Akizungumza na Jambo Tv kwa njia ya simu leo Novemba 17, 2025, Amesema bado uchunguzi unaendelea kutokana na kifo hicho kuhusisha masuala ya jinai.

MC Pilipili alifariki dunia Novemba 16, 2025 jijini Dodoma baada ya kuzidiwa na kisha kupelekwa hospitalini ambako alifika akiwa ameshafariki.