TPLB Yatangaza Tuzo za Ligi Kuu Zitatolewa Disemba 5 – Global Publishers



Dar es Salaam, Tanzania — Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza rasmi kuwa Tuzo za Ligi Kuu za msimu wa 2024/2025 zitatolewa mnamo Disemba 5, 2025, katika ukumbi wa Super Dome Masaki, Jijini Dar es Salaam.

Tuzo hizo zinatarajiwa kuwa heshima na pongezi kwa wanamichezo, makocha na wadau wengine wa ligi waliyeonyesha kiwango bora na mchango mkubwa katika nyanja mbalimbali za michezo msimu uliopita.

Kwa mujibu wa TPLB, hafla hiyo ni sehemu ya jitihada za kuenzi vipaji na kuongeza motisha kwa wachezaji na timu katika ligi kuu ya Tanzania Bara. Washindi watapewa tuzo zinazojumuisha zawadi, medali na heshima za kipekee kutokana na michango yao katika maendeleo ya ligi.

Bodi ya Ligi Kuu imetoa mwaliko kwa wadau wote wa soka nchini, mashabiki na wanahabari kushiriki katika hafla hiyo ya heshima ya michezo.