Rais Samia Amteua Lazaro Nyalandu Kuwa Balozi – Global Publishers



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Samuel Nyalandu, kuwa Balozi.

Taarifa hiyo imetolewa leo, Jumatano tarehe 19 Novemba 2025, na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi kupitia Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses M. Kusiluka.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Samuel Nyalandu, kuwa Balozi.

Hata hivyo, taarifa hiyo haikufafanua Nyalandu atapangiwa kituo gani cha kazi, ikielezwa kuwa ataapishwa na kupangiwa majukumu yake baadaye.

Lazaro Nyalandu aliwahi kushika majukumu mbalimbali ya uwaziri na ubunge, na uteuzi wake kama Balozi unaongeza sura mpya katika safari yake ya kisiasa na ya utumishi kwa taifa.