WAZIRI MPYA WA FEDHA, MHE. BALOZI KHAMIS MUSSA OMAR AWASILI OFISI ZA WIZARA YA FEDHA

Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akizungumza jambo baada ya kukabidhiwa nyaraka na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (hayupo pichani), ambazo ni miongozo mbalimbali za utendaji wa Wizara, katika ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square jijini Dodoma. Mhe. Balozi Omar aliambatana na Naibu Mawaziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) na  Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb) (hawapo pichani).

Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (Kushoto), akiteta jambo na   Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, mara baada ya kufika ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Sqauare jijini Dodoma, ambapo aliambatana na Naibu Mawaziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) na Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb).(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma) 

Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (Katikati), baada ya kukabidhiwa nyaraka na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, ambazo ni miongozo mbalimbali za utendaji wa Wizara, katika ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square jijini Dodoma. Mhe. Balozi Omar aliambatana na Naibu Mawaziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) (wa pili kulia), na  Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb) (wa kwanza kulia).