Masauni: Vyombo vya Habari kusaidia kutoa elimu ya Muungano, Mazingira

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema Ofisi hiyo imepanga kupanua wigo wa elimu ya Muungano naMazingira kwa wadau ikiwemo vyombo vya habari.

Amesema hayo wakati wa mazungumzo yake na Viongozi na Menejimenti ya Ofisi hiyo mudamfupi baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. SamiaSuluhu Hassan, Dodoma Novemba 18, 2025.

Mhe. Masauni amesema iwapo vyombo vya habari vina nafasi kubwa yenye umuhimu wakipekee katika kuelimisha, kujenga na kuimarisha mshikamano katika jamii.

“Tutakaa pamoja na wahariri wa vyombo vya habari ili kushauriana na kuweka mikakati yapamoja katika utoaji wa elimu ya Muungano na Mazingira” amesema Mhe. Masauni.

Amesisitiza kuwa utoaji elimu kuhusu Muungano utagusa makundi yote ya kijamii hususanivijana na watoto hatua inayolenga kuimarisha msingi na faida za Muungano.

Aidha Mhe. Masauni amesisitiza wito wa kutolewa kwa elimu hiyo ili jamii iweze kufahamuumuhimu wa Muungano, historia yake pamoja na faida zake.

Kuhusu Mazingira, Mhe. Masauni amesema Serikali imepanga kutumia mbinu na njiambalimbali za utafutaji wa fedha za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

“Suala la mazingira limejikita zaidi katika uhifadhi na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, lakini pia ni sekta mpya ya kiuchumi yenye uwezo wa kuzalisha mapato, ajira, na kukuza pato la taifa” amesema Mhandisi Masauni.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemejaamesema mbali na Muungano na Mazingira pia Uchumi wa Buluu nao utapewa kipau mbelesababu ni eneo ambalo likisimamiwa vizuri litasaidia kuongeza pata la taifa.

Amesema elimu ikitolewa vizuri na jamii ikaelewa kuhusu Uchumi wa Buluu itasaidia vijanakupata ajira na kuongeza vipato kwa wananchi na mwisho wa siku kila mmoja anakuwa nawajibu katika Utunzaji na Uhifadhi wa mazingira.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Hamad Yussuf Masauni(kushoto) akipokea nyaraka na machapisho mbalimbali kutoka kwa Katibu Mkuu waOfisi hiyo Mhandisi Cyprian Luhemeja mara baada ya kuwasili katika Ofisi hizoMtumba Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja (aliyesimama) akiwakaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (katikati) na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Festo Dugange (kulia) mara baada ya kuwasili ofisini, Novemba 18, 2025.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni(katikati), Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Festo Dugange (kulia) pamoja na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Mhandisi. Cyprian Luhemeja wakiwa katikapicha ya pamoja mara baada ya Waziri na Naibu Waziri kuwasili katika Ofisi hiyo, Novemba 18, 2025.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauniakiongea na baadhi ya Viongozi pamoja na Menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Raismara baada ya kuwasili katika Ofisi hiyo. Kulia kwake ni Naibu Waziri Ofisi yaMakamu wa Rais Mhe. Dkt. Festo Dugange na Kushoto kwake ni Katibu Mkuu waOfisi hiyo Mhandisi. Cyprian Luhemeja.