Rais Samia na Rais Museveni Watunukiwa Tuzo za Heshima na CAF – Global Publishers



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, wametunukiwa tuzo za heshima na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa kutambua mchango wao mkubwa katika maendeleo ya michezo barani Afrika.

Tuzo hizi zimetolewa katika hafla ya utoaji tuzo za CAF iliyofanyika mjini Rabat, Morocco, ambapo mchango wa viongozi hao wawili katika kukuza soka na michezo kwa ujumla ulitambuliwa rasmi.

Kwa niaba ya Rais Samia, tuzo hiyo ilipokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, akiishikilia heshima ya taifa mbele ya viongozi na mashirika ya michezo yaliyohudhuria hafla hiyo.

Hii ni ishara ya kuenzi juhudi za viongozi wa Afrika katika kukuza michezo kama chachu ya maendeleo ya vijana na ukuaji wa soka barani.