Wito huo umetolewa na Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa
Pwani, Bw. Albert Machua, wakati wa kikao kazi cha kuwakaribisha Taasisi ya
Watu wenye Ulemavu Peace Life for Persons with Disability Foundation (PLPDF).
Bw. Machua amesema mradi huo unalenga kuwawezesha wasichana,
wanawake na vijana wenye ulemavu kiuchumi na kimaendeleo, ambapo utekelezaji
wake utaanza katika wilaya za Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa PLPDF Bi. Sophia Mbeyela
amesema mradi huo utatoa elimu ya maisha, ujasiriamali na uelewa kuhusu mkataba
wa kimataifa wa haki za watu wenye ulemavu (ADB), huku wakitarajia kuwafikia
zaidi ya watu wenye ulemavu mia moja ili kuongeza uhamasishaji katika jamii.
Naye Wakili Gidion Mandesi ameeleza kuwa mkataba wa ADB
unaelekeza ulinzi na haki za watu wenye ulemavu katika maeneo mbalimbali,
ikiwemo upatikanaji wa huduma, elimu na fursa sawa katika jamii.






