Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa ushindi wa kishindo aliyoupata katika Uchaguzi Mkuu, Oktoba 2025.
Makamu wa Rais ametoa pongezi hizo wakati akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Zanzibar. Amesema ushindi huo ni matokeo ya kazi kubwa aliyofanya Dkt. Mwinyi pamoja na Chama Cha Mapinduzi katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Kwa upande wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amempongeza Makamu wa Rais Dkt. Nchimbi, kwa kushika wadhifa huo, na kumuhakikishia kuendelea kufanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Makamu wa Rais katika kutafuta ufumbuzi wa masuala mbalimbali ya kimuungano.
Makamu wa Rais Dkt. Nchimbi, amefanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa lengo la kujitambulisha.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
22 Novemba 2025
Ikulu – Zanzibar.

.jpeg)
.jpeg)


.jpeg)